Ulimwengu wa Habari


  • Tafuta
      • Lolote
      • Yote
      • Kamili
MHANDISI ALIYESHINDWA KUWAJIBIKA LUDEWA APELEKWA RUKWA KWA WAZIRI MKUU PINDA .
01/26/2012, 01:51:14 AM  Imeonwa mara: 59  
Sakata ya ubovu wa miradi ya ujenzi wa barabara na nyumba za watumishi katika wilaya ya Ludewa limechukua sura mpya baada ya mhandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya Ludewa Rashid Mtamila kushushwa cheo na kuondolewa katika wilaya ya Ludewa na kupelekwa katika mkoa wa Rukwa kama ambavyo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe alivyoomba mhandisi huyo kupelekwa huko ili kubanwa zaidi na waziri mkuu Mizengo Pinda.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo ya Ludewa wamempongeza naibu waziri huyo Mwanri kwa kufanya kweli tofauti na wengi walivyofikiri kuwa wenda kauli zake zilikuwa ni nguvu ya soda na hivyo kumpa pongezi kwa kuwa kiongozi mtendaji na mtekelezaji wa kauli zake.


Habari za uhakika kutoka Ludewa zinadai kuwa tayari mhandisi huyo Mtamila amepewa barua ya kushushwa cheo na kutakiwa kuondoka katika wilaya ya Ludewa na kwenda mkoani Rukwa ambako ni mkoa anaotoka waziri mkuu Mizengo Pinda.

Mtamila anadaiwa kushindwa kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Ludewa ikiwemo nyumba ya mganga wa kituo cha afya Lupanga ambayo mbali ya kutokamilika imeanza kubomoka ujenzi pia ujenzi wa nyumba zaidi ya 10 za watumishi uliotumia zaidi ya shilingi milioni 200 ila nyumba hizo kabla ya kuanza kutumika zimeanza kubomoka , ujenzi wa barabara kujengwa chini ya kiwango.

Hali hiyo ilimlazimu mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kumwomba naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kumwondoa mhandisi huyo Mtamila na mwenzake wa umwagiliaji katika wilaya hiyo Christopha Nyandiga kwa madai kuwa Ludewa hawatakiwi labda wapelekwe jimboni kwake Mwanri ama mkoa wa waziri mkuu Pinda ili kubanwa zaidi .
mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.


Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.

“Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “

Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .

Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi .

Kitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.

Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2

Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo.

Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.
 
 Maoni
   
Hakuna maoni yaliyowekwa habari. click here uwe mtu kwanza kuweka maoni.
 
 
 
 
 
Tuma: 
 
Powered By Nice News Script