Ulimwengu wa Habari


  • Tafuta
      • Lolote
      • Yote
      • Kamili
MHANDISI AJAZA MAJI KTK TANKI KUFICHA SIRI, LUDEWA.
01/18/2012, 09:33:50 AM  Imeonwa mara: 58  
Na Francis Godwin,Ludewa

MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe asema mhandisi wa maji katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Christopher Nyandiga amemdanganya naibu waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri kwa kujaza maji katika tanki linalotumiwa na wananchi wa mji wa Ludewa ili Kumdanganya naibu waziri huyo kwamba wananchi wa Ludewa Mjini hawana kero ya maji.

Naibu Waziri alipofika kwenye tenki hilo alionyeshwa tenki kubwa lililojaa maji pomoni huku maji mengine yakimwagika, hali ulitumia matumaini mhe. Waziri kwamba Ludewa wananchi wa Ludewa Mjini wana 'surplus' ya maji, kitendo ambacho mbunge Filikunjombe alikipinga.

Lengo la mhandisi huyo kujaza tanki hilo maui ni kutaka kumwonyesha naibu waziri huyo kuwa Ludewa kuna maji mengi na wananchi hawana shida ya maji pia kujisifu kwa mradi huo mzuri.



Hatua ya mbunge huyo kubaini udanganyifu huo ilitokana na kilio cha wananchi wa mji wa Ludewa kupeleka malalamiko Yao dhidi ya kero ya maji katika mji huo na kuwa baada ya ziara ya naibu waziri huyo maji yalikuwa yakitoka kutwa nzima na baada ya msafara wa naibu waziri Kwenda kukagua maji eneo la Mdonga mji nzima ulikuwa hauna maji.

Mbunge huyo alisema mhandisi huyo alifunga maji kwa mud a wa Siku tatu ili kuliwezesha tanki Hilo kujaa maji na waziri huyo alipotembelea kukagua mradi huo alikuta maji yamejaa kupita kiasi katika tanki Hilo huku yakimwagika jambo lililomfanya naibu waziri huyo kuamini.

Alisema kuwa sababu ya kumwomba naibu waziri Mwanri kumpa katibu wake ili Kwenda kutazama mradi huo juzi majira ya jioni na kukuta tanki hilo kavu halina maji .

Mbunge huyo alisema kuwa kitendo cha mhandisi huyo wa wilaya kufunga maji kwa mud a wa Siku tatu ili kutaka kumdanganya naibu waziri huyo si cha kimaendeleo bali ni kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa Ludewa.

"kweli kumdanganya waziri kiasi hiki ni saw a na kumdanganya Rais Jakaya Kikwete ambae amemteua naibu waziri huyo jambo ambalo halipaswi kuvumiliwa "

Alisema kuwa si kweli Kama Ludewa mji wananchi wake wamekuwa walipata maji mud a wote na kuwa moja Kati ya kilio cha wananchi wa mji wa Ludewa ni kupata maji safi ya uhakika .

Kwa upande wake wananchi wa mji wa Ludewa walipongeza hatua ya mbunge wao kufichua udanganyifu huo ambao naibu waziri alifanyiwa na mhandisi huyo wa maji Ludewa Bw .Nyandiga na kuomba TAMISEMI Kuwakataa mahandisi mwenye moyo wa kufanya kazi alisema Jonh Haule

Kwa upande wake naibu waziri huyo Mwanri alisema kuwa ujanja uliofanywa na mhandisi huyo Nyandiga katika kuficha ukweli wa mradi huo wa maji ni ujanja ambao alipata kuugundua wakati alipotembelea mradi huo ila dawa dhidi ya mhandisi huyo ipo jikoni na hatadumu katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa hawezi kuacha fedha za serikali zinazotolewa kwa jail ya miradi ya maendeleo zinatafunwa na mchwa wachache katika Halmashauri kama ilivyo katika Halmashauri hiyo ya Ludewa.

Mwanri alisema mhandisi huyo ni vema atambue kuwa kwa utendaji huyo lazima akubali kuondolewa kutokana na kushindwa kazi na kuwa malipo ya udanganyifu na hujuma ya fedha za miradi ya maji ni kuwajibishwa.

Pia Mwanri aliwataka madiwani wa Halmashauri hiyo ya Ludewa kutoendelea kunyamaza kimya na kuacha miradi ya maendeleo ikitafunwa na wajanja wachache.

Mwandishi wa habari hizi alipomfuata Mhandisi Nyandiga kwa ajili ya kuelezea zaidi juu ya mradi huo wa maji ulitumia fedha za serikali zaidi ya shillingi millioni 30 bila kufanya kazi kwa uhakika alisema yeye si msemaji wa Halmasahauri hiyo na hawezi zungumzia suala hilo.
 
 Maoni
   
Hakuna maoni yaliyowekwa habari. click here uwe mtu kwanza kuweka maoni.
 
 
 
 
 
Tuma: 
 
Powered By Nice News Script