shwari dot com Habari,east african news, Tanzania news, uganda news, kenya news,ethiopians news, somali,swahili news, habari za kiswahili,habari za kenya, http://www.shwari.com/ulimwengu MAJAMBAZI WAVAMIA ENEO LA MLIMANI CITY DAR USIKU HUU Jiji la Dar es salaam limezidi kugubikwa na wimbi la ujambazi wa kutumia pikipiki za miguu k maarufu kwa jina la bodaboda, Ikiwa ni majira ya saa nne kamili usiku huu limetokea tukio la aina yake la ujambazi wa kimya kimya.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka jijini D,Salaam Andrew Mwamasangula anaripoti kwa tukio hilo limetokea katika kituo cha mafuta cha total kilichopo maeneo ya mlimani city

Majambazi hao wakitumia pikipiki mbili waliingia kama wateja na kuwateka walinzi wenye silaha kisha kuwateka wahudumu kwa mtindo wa kimyakimya bila kurusha risasi. Waliwasachi walinzi na wahudumu hao na kuwaamuru walale chini na ndipo walipochukua fedha na kutokomea wakielekea Mwenge.

Katika eneo la tukio kulikuwepo na tax (iliyosajiliwa) pikipiki ya miguu mitatu maarufu bajaj na hizo pikipiki mbili za majambazi. Dereva wa bajaji alionekana kukaidi kulala na alichapwa kibao kilichomfanya alale chini mwenyewe na yeye kusachiwa. Inavyoonekana ni kiwango kikubwa cha fedha walizobeba kwa jinsi walivyobeba ile mifuko.
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/M_J_M_ZI_W_V_MI_N_M_IM_NI_ITY_D_U_I_U_UU.aspx 02/17/2012, 04:28:20 AM
MWANRI AWASHA MOTO KWA MHANDISI WA KILOLO - IRINGA NAIBU waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Agrrey Mwanri ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kumwandikia barua mkandarasi aliyejengwa barabara yenye urefu wa kilomita 2.5 kwa thamani ya zaidi ya milioni 70 kurudia ujenzi wa barabara hiyo iliyopo eneo la Kilolo mjini baada ya kujengwa chini ya kiwango.

Mwanri ambaye ni mbunge wa jimbo la Hai akitoa agizo hilo Leo baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo wakati wa mwendelezo wa ziara yake mkoani Iringa ziara yenye lengo la kuhakikia ubora wa miradi ya Halmashauri ambayo inatekelezwa kwa fedha za kodi za wananchi .

Alisema kuwa pamoja na kuwa barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha changarawe ila bado upo uwezekano mkubwa wa barabara hiyo kuharibika kabla ya mwaka mmoja kumalizika kutokana na mkandarasi kushindwa kujenga makaravati ya kutosha wala kuchimba mifereji ya kupitisha maji ya mvua zaidi ya kuacha maji kupita juu ya barabara jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa barabara hiyo.

Aidha Mwanri amemuonya vikali mhandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana kuhakikisha anasimamia vizuri miradi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo na iwapo atashindwa kufanya hivyo atawajibishwa.

Kwani alisema inashangaza kwa mhandisi huyo wa ujenzi katika wilaya ya Kilolo kukabidhi fedha zote kwa mkandarasi huyo huku barabara hiyo ikiwa imejengwa chini ya kiwango na kuwa kufanya hivyo ni kuonyesha kushindwa kusimamia ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo.

"Napenda kuwaagiza sasa mkurugenzi wa Halmashauri na mwenyekiti wa Halmashauri kukaa chini na kumwandikia Barua mkandarasi aliyejenga barabara hii Mara moja afiki kurudia kukamilisha ujenzi wa barabara hii ....haiwezekani Kabisa barabara kujengwa bila kuweka mifereji ya kutolea maji ya mvua ....sasa ujenzi huu ni saw a na hakuna .....nasema sikubaliani na ujenzi huu naomba urudiwe haraka"alisisitiza Mwanri.
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/MW_N_I_W_M_T_W_M_NDI_I_W_I_-_I_ING_.aspx 02/17/2012, 04:26:05 AM
MWEKEZAJI KAPUNGA MBARALI MBEYA AFIKISHWA MAHAKAMANI
SERIKALI imemfikisha mahakamani Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kampuni ya Expotr Trading Group amefikishwa mahakama ya wilaya ya Mbeya kwa makosa mawili tofauti likiwemo kosa la kula njama la kutenda kosa la kuharibu mali na kuharibu mali za wananchi kwa hila.

Mwekezaji huyo alifikishwa mahakamani hapo jana kwa makosa hayo aliyoyatenda  Januari 12 hadi 14, mwaka huu kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa ambapo alimwaga sumu katika mashamba ya wakulima zaidi ya 154 wa Kijiji cha Kapunga wilayani humo.

Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Seif Kulita, Mwendesha mashitaka wa Serikali Griffin Mwakapeje alisema kuwa washitakiwa hao aiwemo Meneja wa shamba hilo Walder Vermaak, Afisa ugani Serger Bekker na Rubani wa ndege Andries Daffe walitenda kosa hilo wilayani humo na kuharibu mazao ya wakulima hekari 489.5.

Mwakapeje alisema kuwa wawekezaji hao wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 226 (i) cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002 la kuharibu mazao hayo ya Mpunga wa wakulima wanaolima eneo linalojulikana kwa jina la Mpunga moja.

Baada ya mashitaka hayo, Hakimu Kulita alpowauliza washitakiwa hao wote kwa pamoja walikana shitaka hilo ambapo wakili anaowatetea watuhumiwa hao Ladislaus Rwekaza aliomba dhamana kwa wateja wake na hatimaye mahakama ikaridhia kwa Masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja mweye mali isiyohamishika isiyopungua Shilingi Milioni kumi.

Aidha Hakimu huyo alitoa sharti kwa watumumiwa hao kuwa mbali na sharti la kuwa na mdhamini mmoja na mali isiyohamishika pia watuhumiwa waliytakiwa kukabidhi hati za kusafiria na kwamba hawapaswi kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya na kama watahitaji kusafiri nje ya mkoa wa Mbeya ni lazma wapate kibali cha mahakama hiyo ambapo washitakiwa walitimiza masharti hayo.

Baada ya Masharti hayo watuhumiwa walidhaminiwa na Uwesu Msumi mkazi wa Jijini Dar Es Salaam na kukabidhi hati ya nyumba yenye namba 229 Block J iliyopo Mbezi Jijini Dar es Salaam, Christian Basil Mmas aliyekabidhi hati ya nyumba yenye namba 109 iliyopo Geza Ulole Jijini Dar es Salaam na Sunnil aliyetoa hati namba 254 iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kesi hiyo itatajwa tena Machi 6, mwaka huu.


Baadhi ya wananchi walioathiriwa na sumu hiyo wakati ndege ikimwaga mashambani na kushuhudiwa ni pamoja na Michael Shija, Severina Mbwilo, Elikana Nsemwa, Edward Simkoko, Gaidon Peter Ngogo (54), Jailo Esau (22), Jackson Mwandemange  (52), Catherina Shipela (50), Edda Ngosha (35), Julius Isega(50), Ramadhan Nyoni (52)
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/MW_Z_JI_PUNG_M_I_M_Y_FI_I_W_M_M_NI.aspx 02/15/2012, 11:11:03 AM
MWANRI AWAJIA JUU MADAKTARI WANAOWAUZIA DAWA AKINA MAMA WAJAWAZITO

NAIBU waziri wa serikali za mitaa na tawala wa mikoa (TAMISEMI )Agrrey Mwanri ameagiza uongozi wa wilaya ya Iringa kufuatilia wauguzi wa Hospital ya mkoa wa Iringa na vituo vya afya katika manispaa ya Iringa vinavyowauzia dawa wanawake wajawazito pindi wanapokwenda kujifungua.

Mwanri alitoa agizo hilo jana alipokuwa akipokea maswali ya wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wake uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa hadi majira ya saa mbili za usiku .

Alisema kuwa serikali ilitangaza huduma za bure kwa mama mjamzito pindi anapokwenda kujifungua na kuwa mahitaji yao yote yanagharamiwa na serikali hivyo anashangazwa na kuwepo kwa utaratibu huo wa wauguzi wa Hospital zaserikali kuwaagiza wagonjwa hao kutoa baadhi ya gharama ili kufanikisha hudumaza kujifungua .

Mwanri alisema kuwa iwapo wauguzi hao wanafanya hivyo ni kosa kubwa nakwenda kinyume na maagizo ya sera ya afya inayotaka akina mama wajawazitokupatiwa huduma za bure za matibabu .

Hivyo aliunda tume maalum ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Aser Msangi kuchunguza madai hayo na kabla ya kuondoka apate jibu ili aweze kutoa adhabu kali kwa wahusika.

Aidha Mwanri aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Iringa kupitia wanasheria wake kufuatilia sakata la wazazi wa shule ya sekondari Lugalo mjini hapa kuchangishwa fedha za kununua basi zaidi ya milioni 15 na fedha hizo kuliwa na mmoja kati ya watumishi wa shule hiyo.

Katika hatua nyingine naibu waziri huyo alieleza kusikitishwa na ubovu wa barabara ya Kigonzile katika manispaa ya Iringa na kutaka manispaa ya Iringa kuifanyia kazi kero hiyo.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ulimtafuta kwa njia ya simu mganga mkuu wa Hospital ya mkoa wa Iringa Dr Ezekiel Mpuya ili kutolea ufafanuzi wa madai hayo ambapo alidai kuwa hakuna ukweli wowote na kuwa anachotambua wajawazito wote wanapatiwa huduma za bure katika Hospital hiyo.

Japo alisema kuwa tatizo la Hospital hiyo kukosa dawa lilipata kujitokeza mwaka jana mwezi wa 12 na kuwa hapo kidogo wajawazito walipata shida ya kutafuta dawa ila tatizo hilo serikali imelifanyia kazi na sasa hakuna tatizo tena.

http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/MW_N_I_W_JI_JUU_M_D_T_I_W_N_W_UZI_D_W_IN_M_M_W_J_W_ZIT_.aspx 02/15/2012, 10:56:36 AM
WAKAZI WA KIJIJI CHA KAPUNGA - MBARALI MKOANI MBEYA WAMEINGIA HASARA YA SHILINGI MILIONI 718.
Habari na Mbeya yetu blog.
Wakazi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameingia hasara ya shilingi milioni 718 kutokana na mwekezaji wa mashamba ya Kapunga rice project kumwaga sumu ya kuua mimea, kwa kutumia ndege.

Mwekezaji huyo alifanya tukio hilo Januari 12 hadi 14, mwekezaji kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa alimwaga sumu hiyo katika mashamba yake, pia na katika mashamba ya wananchi katika eneo linalofahamika kwa jina la Mpunga mmoja, na kusababisha wakulima zaidi ya 154, wanaomiliki zaidi ya hekari 494 na heka 5.

Meneja Mkuu wa shirika la Kapunga Rice Project Wally Vermaak amesema ataendelea kufanya hivyo hadi hapo wananchi hao watakapo acha kutumia ardhi anayoimiriki.

Hadi sasa ni wananchi Baadhi ya wananchi 8 akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Raphael Moreli mwenye umri wa miaka 44 wameshaathirika na sumu hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mbarali Luteni Kosimasi Kayombo amesema tume aliyoiunda kuchunguza tukio hilo bado inaendelea na uchunguzi.
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/W_ZI_W_IJIJI_PUNG_-_M_I_M_NI_M_Y_W_M_INGI_Y_I_INGI_MI_I_NI_718.aspx 02/08/2012, 10:39:58 AM
NMB BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI - MBEYA
Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa msaada wa madawati mia moja na kumi yenye thamani ya shilingi kwa shule za msingi Sinde, Maanga, Lyoto na Ilomba ili kuboresha huduma za elimu kwa shule hizo.

Akikabidhi msaada huo wa madawati meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lukesia Bena amesema benki yake imetoa msaada huo baada ya kuridhia ombi lililotolewa na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kwa benki hiyo kusaidia madawati kwa shule za msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi kupenda masomo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Mbeya Afisa elimu wa shule za msingi jiji Bi.Aurelia Luensi ametoa shukrani kwa uongozi wa Benki hiyo kuchangia katika elimu na kuwasihi walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo.

Naye mwakilishi wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ambaye ni diwani wa kata ya Sinde Fanuel Kuanula amesema misaada hiyo imefika kwa wakati muafaka ambapo wanafunzi wanauhitaji mkubwa wa madawati kutokana na yale yaliyopo kuchakaa.

Shule ya msingi Sinde imepata madawati 34, Lyoto 36, Ilomba 15 na Maanga 28.

HABARI NA MBEYA YETU
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/NM_N_Y_T_M_D_W_M_D_W_TI_-_M_Y_.aspx 02/08/2012, 10:37:05 AM
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MWANZA CHAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 10

Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza kimekusanya kiasi cha sh. Milioni kumi laki tisa na elfu sabini (1797,0000)kutokana na makosaya kiusalama .

Mwandishi wa mzee wa matukio daima kutoka Mwanza Abas Dominic anaripoti kuwa hayo yamesemwa na jeshi la plisi mkoani humo wakati wa kikao cha na vyombo vya habari ambapo kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Liberatus Ballow amesema fedha hizo zimepatikana kutokana na jumla ya makosa elfu kumi na kumi natisa (1019)yaliyotokea ndani ya wiki moja.

Kuusu kuwepo kwa maazimisho ya miaka (35) tangu kuzaliwa kwa chama cha CCM itakayo fanyika tarehe 5.2.2012 mkoani humo amesema wamejipanga kikamilifu ili kuakikisha wageni pamoja na raia wanasherehekea vizuri nakuongeza kuwa watareta maasikali wengine kutoka Misungwi kwa ajili ya zoezi hilo la usalama.

Hivyo amewataka wenyeji wa mkoa wa Mwanza kuwapokea wageni vizuri kwasababu kuwepo kwa sherehe hiyo kutawaingizia kipato wenyeji katika uzalishaji wao.

http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/_I_I_U_M_NI_MW_NZ_U_NY_Z_IDI_Y_MI_I_NI_10.aspx 02/04/2012, 11:31:03 AM
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NDANI AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI WA MBEYA AMANI

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi SHAMSI VUAI NAHODHA amewahakikishia wananchi wa mbeya kuwa wizara yake kupitia jeshi la polisi limejipanga kupunguza ama kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu vikiwemo vya upikaji nondo vilishamiri mkoani Mbeya.


NAHODHA ameyasema hayo mkoani Mbeya akizungumza na waandishi wa habari,kwamba vitendo vya kiahalifu vinavyojitokeza mara zote mkoani Mbeya vitakwisha tu ikiwa wananchi wataonesha ushirikiano wa dhati kwa askari wa jeshi la polisi kwani wanaofany avitendo hivyo wanajulikana.


Kwa taarifa zaidi na Hosea Cheyo Kwa kuwa wananchi wanaoishi, na kuingia mkoani Mbeya wamekuwa na hofu na wasiwasi dhidi ya vitendo vya kihalifu vikiwemo vya upigaji wa nondo watu vinavyotokea mara kwa mara mkoani humo,Waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kueleza mipango ya kufikia suluhisho.



Nahodha ambaye pamoja na mambo mengine amefika mkoani Mbeya kukagua shughuli za wizara yake,lakini amezungumzia namna ya kushughulikia suala la wahamiaji haramu na kueleza msitakabali ya watendaji wake kuwa kuna mabadiliko yanafanyika katika idara ya uhamiaji nchini.

http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/W_ZI_I_W_M_M_Y_ND_NI_Y_ND_NI_M_W_I_I_I_W_N_N_I_W_M_Y_M_NI.aspx 02/04/2012, 12:23:02 PM
MHANDISI ALIYESHINDWA KUWAJIBIKA LUDEWA APELEKWA RUKWA KWA WAZIRI MKUU PINDA . Sakata ya ubovu wa miradi ya ujenzi wa barabara na nyumba za watumishi katika wilaya ya Ludewa limechukua sura mpya baada ya mhandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya Ludewa Rashid Mtamila kushushwa cheo na kuondolewa katika wilaya ya Ludewa na kupelekwa katika mkoa wa Rukwa kama ambavyo mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe alivyoomba mhandisi huyo kupelekwa huko ili kubanwa zaidi na waziri mkuu Mizengo Pinda.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya watumishi katika Halmashauri hiyo ya Ludewa wamempongeza naibu waziri huyo Mwanri kwa kufanya kweli tofauti na wengi walivyofikiri kuwa wenda kauli zake zilikuwa ni nguvu ya soda na hivyo kumpa pongezi kwa kuwa kiongozi mtendaji na mtekelezaji wa kauli zake.


Habari za uhakika kutoka Ludewa zinadai kuwa tayari mhandisi huyo Mtamila amepewa barua ya kushushwa cheo na kutakiwa kuondoka katika wilaya ya Ludewa na kwenda mkoani Rukwa ambako ni mkoa anaotoka waziri mkuu Mizengo Pinda.

Mtamila anadaiwa kushindwa kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Ludewa ikiwemo nyumba ya mganga wa kituo cha afya Lupanga ambayo mbali ya kutokamilika imeanza kubomoka ujenzi pia ujenzi wa nyumba zaidi ya 10 za watumishi uliotumia zaidi ya shilingi milioni 200 ila nyumba hizo kabla ya kuanza kutumika zimeanza kubomoka , ujenzi wa barabara kujengwa chini ya kiwango.

Hali hiyo ilimlazimu mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kumwomba naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kumwondoa mhandisi huyo Mtamila na mwenzake wa umwagiliaji katika wilaya hiyo Christopha Nyandiga kwa madai kuwa Ludewa hawatakiwi labda wapelekwe jimboni kwake Mwanri ama mkoa wa waziri mkuu Pinda ili kubanwa zaidi .
mbunge wa jimbo la Ludewa acharuka mbele ya naibu waziri amkataa mhandisi wa maji na mhadisi wa ujenzi ataka naibu waziri kuwapeleka jimboni Kwake ama jimbo la waziri mkuu Mizengo Pinda.


Mbunge Filikunjombe alimweleza naibu waziri huyo kuwa wilaya ya Ludewa imegeuzwa kuwa ni shamba la bibi kwa baadhi ya viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia vibaya nafasi zao kwa kuhujumu miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa kila wakati amekuwa akiwaonya watumishi wa wilaya ya Ludewa kufanya kazi yao kwa uadilifu ila baadhi yao wameshindwa kabisa kuonyesha uaminifu katika utendaji wa kazi yao.

“Viongozi wenzangu na madiwani wangu wapo walionifuata kutaka niwatetee kwa uozo huu ila nasema heri kulaumiwa kwa kusimamia ukweli na kupinga ufisadi unaofanyika katika wilaya ya Ludewa ila nipo tayari kuendelea kufanya kazi na viongozi waadilifu “

Alisema kuwa wahandisi hao wameendelea kuwa kikwazo kikubwa katika wilaya ya Ludewa na kuwa miradi mbali mbali inayosimamiwa katika wilaya hiyo imekuwa ni mibovu na haina sifa japo imetumia fedha nyingi zaidi .

Mapema asubuhi naibu waziri huyo alifanya ziara ya ghafla ambayo haikuwepo katika ratiba katika banio la mradi wa umwagiliaji wa Lifua ambalo umejengwa na kampuni ya Summer Communication kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 357 toka mwaka 2009/2010 bila kufanya kazi .

Kitoa taarifa ya mradi huo mbele ya naibu waziri Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Nyandiga alisema kuwa awamu ya kwanza ilitumia kiasi cha shilingi milioni 357,262,990 na mradi huo kukabidhiwa kwa Halmashauri toka mwaka 2010 japo hautumiki kutokana na kuvujisha maji.

Wakati awamu ya pili mradi ulijengwa na kampuni ya Tan Direct Co.Ltd ya Dar es salaam kwa gharama ya shilingi milioni 227,613,136.15 kwa kazi ya kujenga mfereji wenye urefu wa mita 1725,usakafiaji wa eneo la kuingia na kutoka kwenye daraja hilo ,ujenzi wa vigawa maji vinne na ujenzi wa vianguko vya maji vinne na ujenzi wa kivusha maji kimoja na kuwa hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa asilimia 64.9 ya fedha zote na kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 73.2

Akimhoji mkandarasi huyo naibu waziri huyo Mwanri alimtaka kueleza sababu ya kulipa mamilioni ya fedha katika mradi huo bila kufanya kazi na hauna maji katika kipindi hiki cha masika ,mhandisi huyo alikana kuwa yeye si msanifu wa mradi huo hivyo hawezi kujibia swali hilo.

Akitoa majumuisho yake na maombi ya mbunge Filikunjombe ya kutaka wahandisi hao kuondolewa katika wilaya hiyo ya Ludewa naibu waziri huyo alisema suala hilo linawezekana kwani pia kwa upande wake hajapendezewa na ufisadi mkubwa uliofanyika katika miradi hiyo.
http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/Habari_za_kitaifa/M_NDI_I_IY_INDW_UW_JI_I_UD_W_P_W_U_W_W_W_ZI_I_M_UU_PIND_.aspx 01/26/2012, 01:51:14 AM
Kenya’s richest man Uhuru Kenyatta to face ICC trial

By SARA WEBB IN THE HAGUE AND JAMES MACHARIA IN NAIROBI 

UHURU Kenyatta, Kenya’s finance minister and son of the country’s founding president, must stand trial at the International Criminal Court (ICC) for directing a militia to murder and rape after the country’s disputed 2007 election, judges have ruled.

They said three other Kenyans, including former minister William Ruto, must face trial along with Kenyatta for crimes against humanity during post-election violence that killed at least 1,220 people.

The decision yesterday by the Hague-based ICC is likely to have far-reaching consequences for the corruption-prone country where a powerful political elite has long been considered almost above the law.

Both Kenyatta, who was ranked Kenya’s richest man by Forbes magazine, and Ruto, a former higher education minister, plan to run for president in an election due by March next year, and the ruling could hurt their ambitions.

Kenyatta protested his innocence last night. “I would like to reiterate before the people of Kenya and before the entire world … that I am innocent of all the accusations that have been levelled against me,” he said in a statement on his Facebook page.

Ruto said he found the ruling strange, would appeal against it and run for president anyway.

The ruling could lead to demonstrations in Kenya, although there were no immediate outbreaks of protest in Kenyatta’s constituency, nor in Ruto’s Rift Valley powerbase.

There are two Kenyan cases at the ICC, split broadly between the ethnic Kalenjin and Kikuyu camps involved in much of the violence. Ruto is a Kalenjin and Kenyatta is a Kikuyu, Kenya’s largest ethnic group.

The ICC’s decision could backfire on another presidential contender, prime minister Raila Odinga, who is accused by Kenyatta and Ruto supporters of trying to exploit the criminal charges for his own political gain.

Kenyan radio presenter Joshua arap Sang and the head of Kenya’s civil service Francis Muthaura must also stand trial, the ICC judges ruled.

Some victims welcomed yesterday’s ruling, while others said the courts should be trying the people who carried out the attacks that drove hundreds of thousands from their homes.

“Justice has been done,” said Harrisson Macharia, whose daughter was killed when a mob of machete-wielding Ruto supporters herded women and children into a church and set it ablaze on New Year’s Day 2008.

“We want justice for everyone who was victimised by the violence,” he said. “We victims are now satisfied with the outcome. We suffered a lot, and we are now waiting for the trial.”

None of the suspects was in court for the half-hour hearing, at which presiding judge Ekaterina Trendafilova read out a summary of the decision to commit four suspects for trial on charges including murder, persecution and deportation.

The suspects will remain free in Kenya until the trials start, but Ms Trendafilova warned they could face arrest if they attempt to whip up fresh violence.

http://www.shwari.com/ulimwengu/Category/_abari_za_ast_fri_a/_nya’s_ri_st_man_U_uru_nyatta_t_fa_I_trial.aspx 01/24/2012, 12:41:07 PM